ITAKUFAIDIA NINI?


Marko 8: 36

 Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake?

(For what shall it profit a man, if he shall gain the whole world, and lose his own soul?)

Itakufaidia nini Kuendelea Kuishi katika Dhambi na Uovu na Kisha kupoteza nafsi yako Kwenye ziwa la moto milele.?

Itakufaidia nini kuendelea kuwa rafiki wa dunia na kuwa adui wa Mungu?

Itakufaidia nini kumkosa Mungu milele kisa huyo kijana/binti anaye kukosesha ufalme?

Itakufaidia nini Kumkosa Mungu kisa dhambi ya Siri unayo endelea kuitenda na hutaki kuchukua Hatua ya kutubu?

Itakufaidia nini kuendelea na kazi inayo kufarakanisha na MUNGU na kukosana na MUNGU

Itakufaidia nini kuendelea Kulikosesha kundi la Bwana kwa mafundisho potofu ya kuwatia moyo kutenda uovu, Huku nafsi zao na mioyo yao inaangamia dhambini na kukaukiana kila siku?

*Nakupa Shauri Leo ;*

Rejea, Rejea ,

Geuka Geuka,

Ondoka kwenye Comfort zone inayo endelea kutafuna nafsi yako na kuendelea kukauka.

Mdo 3:19 _Tubuni basi mrejee, ili dhambi zenu zifutwe , zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana_

MAOMBI

*Asanthe MUNGU Kwa Neema Yako ya Wokovu. Narejea Kwako. Naomba Neema Yako Inifundishe Kukataa Ubaya na tamaa za Kidunia na Kuishi maisha ya haki na utauwa, katika Ulimwengu wa sasa.*

*Kwa Jina la Yesu*

*Ameeen*

🗣Bring

Jesus Christ

To All Nations🌐

www.lifespeakingministry.blogspot.com

No comments:

Post a Comment