USIKAE NA NURU PEKE YAKO



Usikae na NURU peke yako, Wakati Mwingine yupo Gizani.
Huo sio moyo wa YESU.

Usikae na NURU Kwenye Familia yako tu.Wakati Familia ya watu wengine ipo gizani.
Huo sio moyo wa Yesu.

Usikae na NURU kwenye ofisi yako tu.Wakati ofisi ya Ndugu yako ipo gizani.
Huo sio moyo wa Yesu.

Usikae na NURU kwenye Kanisa lako tu . Wakati makanisa mengine yapo gizani.
Huo sio moyo wa Yesu.

Usikae na NURU kwenye maisha yako tu. Wakati maisha ya wengine yapo gizani.
Huo sio moyo wa Yesu.

Usikae na NURU kwenye taifa lako tu Wakati mataifa mengine yapo gizani.
Huo sio moyo wa Yesu.




Matthew 5:14, 16
[14] Ninyi ni nuru ya ulimwengu.  Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
[16] Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
 

No comments:

Post a Comment