Utumishi Mwingi na kuhangaika sana kwa ajili ya YESU.

Kuimba kwingi na kushiriki Matamasha mengi.

Kushare Neno na Ujumbe wa Kutia moyo na kuhamasisha akili za watu.

Kusikiliza Nyimbo sana na kushare Nyimbo na video mitandaoni.

Kwenda Kwenye Nyumba za ibada.

Tiketi Ni nini basi


📩Mathayo 5:8
Heri wenye Moyo safi Maana Hao watamwona MUNGU_
*Moyo safi ni tiketi ya Kumwona MUNGU.*
Tiketi nyingine ni nini basi


📩Waebrania 12:14
Tafuteni kwa Bidii kuwa na Amani na watu wote na huo utakatifu ambao hakuna Mtu atakaye Mwona MUNGU pasipo kuwa nao._
*Utakatifu ni tiketi ya Kumwona MUNGU.*
Nifanye nini, Nipate tiketi hiyo


📩Yohana 14:6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi Njia, na Kweli na Uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi.
*Yesu ndio Njia pekee ya kupata tiketi ya Kumwona MUNGU*.
📩1petro1:15,16
Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu
iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;
16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu.
✝MAOMBI✝
_Nakuamini Yesu Nakiri Kuwa wewe ndie Njia,na Kweli na Uzima, na Ya kuwa Ulikufa na ukafufuka kwa ajili ya ukombozi wangu_.
_kwa Jina La Yesu Kristo mimi ni mtakatifu kwa Kuwa wewe ni Mtakatifu.... Ameen_

Jesus Christ
to All nations

No comments:
Post a Comment