KIUMBE KIMPYA(New Creature)



Ninaposema Kiumbe Kipya nina maanisha ni Kiumbe kipya ambacho hakina mfano wake hapo kabla.(No sample).
  Ni uanzishwaji wa maisha au ni mwanzo wa maisha ambayo mtu hajawai kuishi hapo mwanzo, wala hamna mfano wa maisha hayo.
  (Old things are passed away). Maana yake maisha ya kale yamekufa, hayapo tena.
Maana yake hakuna chembe chembe za kale tena. Ni kiumbe Kipya kabisa, Kiumbe Kimpya kabisa. Sadiki maneno haya: Ni kiumbe Kipya Kabisa.
2kor 5:17
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
(KJV::Therefore if any man be in Christ, he is a new creature: old things are passed away; behold, all things become new)
ü  Ndani ya Kristo YESU pekee, ndio unaweza kuwa kiumbe kipya kabisa.
ü  Historia yako mbaya, na Majuto yako yote ya Kale, yanaweza kuzikwa na kuzikika ndani ya krito YESU pekee.
ü  Kama ulishindwa kubadilika na kushinda hali inayo kutesa sasa. Unahitaji kuwa ndani ya Kristo, na hali hiyo itakuwa ukale ulio pita kuanzia leo (old things are passed away) na utaanza mwanzo mpya(all things become new).
MAOMBI
Asanthe MUNGU kwa ajili ya KRISTO YESU Bwana wangu,   Nimeamua kukufata wewe YESU, na Kukaaa ndani yako. Kaa Ndani yangu BWANA. Nakuamini KRISTO YESU kuwa ulikufa na kufufuka kwa ajili ya maisha yangu. Naomba Neema ya Kunisaidia kuenenda katika upya wa uzima. Katika Jina la YESU KRISTO.  Ameen.
Mimi ni Kiumbe Kipya(I am a New Creature

Email: lifespeakers2015@gmail.com||Web: www.lifespeakingministry.blogspot.com

No comments:

Post a Comment